Monday, November 2, 2009

15 wanaswa na tiketi bandia

Futuna Suleman

WATU 15 wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na tiketi bandia za mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye uwanja mkuu wa Taifa, Dar es Salaam.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Liberatus Sabas alisema watuhumiwa hao wamekamatwa siku hiyo ya mechi wakiwa na tiketi hizo bandia.
Sabas aliwataja watuhumiwa hao na miaka yao kuwa ni Kiliza Hamis, 25 (Mbagala), Shabaan Athuman,18 (Kigamboni), Paulo George,18 (Mbagala), Herman Gekimaki, 32, (Tandika), Omary Issa, 25 (Tandika).
Wengine ni Hamis Simbile 28, (Mbezi), Bakari Ibrahim, 38(Mbagala), Fikiri Mohammed,20 (Temeke Mikoroshini), George John, 20 (Temeke Mikoroshini), Rashid Amri, 20 (Mbagala), Mlokozi Peter 35 (Mbagala) na William Joseph 27, (Yombo Vituka).
Watuhumiwa wengine ni Augustino Modest,26(Mbagala), Francis Mbeta 28,(Manzese), Abeid Kilimile 24,(Manzese), Juma Hamza 25, (Ubungo), Jafar Said 27, (Kimara), Hassan Kindamba 47, (Kijitonyama).
Kamanda huyo amesema watuhumiwa hao wanatarajia kufikishwa mahakama ya Temeke kesho ili kujibu mashtaka hayo.
Tatizo la watu kukamatwa na tiketi bandia limekuwa la kawaida katika kila mechi inayozikutanisha timu za Simba na Yanga.
Katika mechi ya April mwaka huu kati ya timu hizo, watu kadhaa pia walikamatwa baada ya kukutwa na tiketi bandia. Katika mechi hiyo, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

No comments:

Post a Comment