Tuesday, November 3, 2009

Benitez kwenye mtihani mwingine, majeruhi kibao

LONDON, England
Liverpool inajiandaa kuingia uwanjani katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Olympique Lyon kesho, huku ikiwa na mashaka kufuatia wachezaji wake 10 kuwa majeruhi na hivyo nafasi ya kucheza kuwa mashakani.
Wakati huo huo, kocha Rafa Benitez anakabiliwa na mtihani mgumu ambao hajawahi kuupata katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwenye dimba la Anfield.
Benitez hatakuwa na kiungo mahiri na injini ya Liverpool Steven Gerrard, na mwenzake Albert Riera, sambamba na walinzi Martin Kelly na Martin Skrtel ambao wote ni majeruhi.
Liverpool imepoteza mechi sita kati saba katika mechi zote za mashindano, ikiwa ni pamoja na kipigo cha mabao 2-1 kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya Lyon wiki mbili zilizopita, na matumaini ya kuvuka hatua ya makundi iko mashakani kama itapoteza mechi kwenye uwanja wa Stade Gerland.
Lyon inaongoza Kundi E ikiwa na pointi tisa kutokana na mechi tatu, na wanaweza kusonga mbele hatua ya mtoano kama watashinda mechi ya kesho.
Fiorentina, wanakumbana na Debrecen kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi sita wakifuatiwa na Liverpool pointi tatu na Hungarians hawana pointi.

Liverpool, walioshinda Kombe la Ligi ya Mabingwa mara tano na kufikia hatua ya robo fainali katika misimu mitatu, haijaonyesha uwezo wowote msimu huu, wakipoteza mechi nane kati ya 16 katika mashindano yote.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Fernando Torres, aliyepumzishwa katika dakika ya 63 pamoja na kufunga bao kwenye mechi ya waliyochapwa mabao 3-1 dhidi ya Fulham, huenda akalazimika kucheza akiwa na maumivu ya misuli aliyoyapata wakati akiiwakilisha Hispania kwenye michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Afrika Kusini.
"Kwa sana tunajaribu kumuangalia, kwa sababu alikuwa mbioni kufanyiwa upasuaji---tunalazimika kumchukua Fernando kwenda naye Lyon kwa vile hatuna chaguo lingine," alisema Benitez wakati akiongea na tovuti ya Liverpool.
Glen Johnson, (msuli ya miguu) Daniel Agger (mgongo), David Ngog (kifundo cha mguu) na Fabio Aurelio (msuli ya miguu), ni miongoni mwa wachezaji ambao leo wako kwenye mashaka ya kucheza.
Jamie Carragher, alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Fulham sambamba na mwenzake Philipp Degen, na baadaye walisema: "Huu ni wakati mgumu, na hakika unaumiza sana. "Tulifanya mambo mazuri wiki iliyopita kwa kuifunga Manchester United, lakini baada ya hapo tumepoteza mechi mbili."Ni lazima tujirekebishe wiki hii, kwa sababu Lyon ni timu ngumu".
Lyon ilirejea kwenye ushindi baada ya kupoteza mechi mbili, lakini iliibuka na ushindi baada ya kuwafunga mahasimu wao wakubwa St Etienne kwa bao 1-0 Jumamosi iliyopita, na wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Ufaransa wakiwa nyuma ya Girondins Bordeaux kwa pointi mbili.

Huenda timu zikawa hivi:
Lyon: 1-Hugo Lloris; 2-Francois Clerc, 3-Cris, 28-Jeremy Toulalan, 20-Aly Cissokho; 17-Jean Makoun, 8-Miralem Pjanic, 10-Ederson; 14-Sidney Govou, 7-Michel Bastos; 9-Lisandro Lopez
Liverpool: 25-Pepe Reina; 2-Glen Johnson, 23-Jamie Carragher, 27-Philipp Degen, 16-Sotirios Kyrgiakos; 22-Emiliano Insua, 20-Javier Mascherano, 4-Alberto Aquilani, 18-Dirk Kuyt; 15-Yossi Benayoun, 9-Fernando Torres


No comments:

Post a Comment