Na Mwandishi Wetu, Jijini
UONGOZI wa mabingwa wa soka nchini, Yanga, umesema hautishwi na kauli za Shirikisho la soka nchini-TFF kuhusu kuwapa adhabu sambamba na watani wao wa jadi Simba kwa kufuatia vigogo hao kuhoji mapato yaliyotokana na pambano lao lililofanyika zaidi ya wiki moja iliyopita.
TFF imesema kuwa itazichukulia hatua kali klabu hizo mbii kwa kile walichodai kuendekeza utamaduni wa kulalamikia mapato kila wakati timu hizo zinapokutana.
Akizungumza na Alasiri mapema leo, Afisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema klabu yake iko tayari kwa adhabu yoyote kutoka TFF. "Tuko tayari, wanaweza kufanya wanavyotaka, lakini ilikuwa ni haki yetu kuhoji mapato," alisema bosi huyo wa habari Jangwani.
"Kama tatizo letu ni kutaka kujua mapato yetu yalikuwaje, basi wafanye hivyo kwa uongozi wote na wala si mtu mmoja.
"Hatujamtuhumu yeyote, na wala hatujasema kwamba TFF wameiba pesa. Rai yetu ni kutaka kupitiwa upya vitabu vya tiketi. Nadhani TFF hawajatuelewa," aliongeza msemaji huyo.
Wakati Yanga, ikisema hayo, watani zao wa Jadi, Simba imeruka 'kimanga' na kudai kuwa haihusiki na wala haijawahi kutoa tamko la kupitia mapato upya tangu wapewe mgawo wao.
"Tuna haki na uhuru wa kuongea, hatufanyi hivyo kwa kusema mambo ambayo hayako. Kwani TFF inajisikiaje kwa kauli yetu?," alihoji.
"Aaah! sisi hatupo huko, kwani ulishawahi kusikia Simba inalalamikia mapato, au inasema kuwa inapitia upya mapato yake?" alisema msemaji wa Simba, Clifford Ndimbo
Ndimbo alisema kwa sasa akili yao haipo kwenye mapato ila wameielekeza kwenye usajili wa dirisha dogo.
"Sisi sasa hivi tupo kwenye mchakato wa kusajili wachezaji, na wala si mapato, labda uzungumzie ishu nyingine na wala si mapato," alisema.
Katika mechi hiyo, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao hao, ambapo kati ya zaidi ya shilingi milioni 400 zilizopatikana, kila klabu iliambulia shilingi milioni 90, huku taasisi hiyo inayosimamia soka nchini ikiingiza mfukoni milioni 110.
REA YATOA MKOPO WA KUJENGA VITUO VYA MAFUTA VIJIJINI
15 hours ago
No comments:
Post a Comment