
RAFA Benitez, leo anatarajia kufanya jaribio la hatari pale atakapowapanga mastaa wake Steven Gerrard na Fernando Torres kwenye mechi dhidi ya Birmingham, huku akijua fika kwamba wachezaji hao bado majeruhi.
Ni maamuzi yanayojaribu kufufua uhai wa Liverpool msimu huu.
Mwenyewe Rafa, ameshakiri wazi kuwa nyota wake hao hawako fiti kucheza kwa muda wa dakika 90 kutokana na wote kukabiliwa na matatizo ya nyonga.
Isitoshe, Rafa anajiandaa kuwapa taarifa makocha wa timu za taifa za England na Hispania kuhusu kutokuwa fiti kwa wachezaji hao kiasi cha kuitwa kwenye vikosi vya timu za taifa vinavyojiandaa kucheza mechi za kirafiki za kimataifa.
Benitez alisema: "Gerrard hayuko sawa sana, lakini tunasubiri kuona iwapo anaweza kucheza dhidi ya Birmingham, au aketi kwenye benchi la wachezaji wa akiba. Lakini tunatambua kwamba hatakuwa fiti.
"Amekuwa akifanya mazoezi na mtu wa viungo, si kwenye timu na nafahamu kwamba daktari wetu alikuwa akiongea na yule wa timu ya taifa ya England kuhusu hali ya mchezaji.
"Iwapo mchezaji hajafanya mazoezi na wenzake kwa muda wa siku 15, hawezi kuwa fiti kwa asilimia 100. Ataweza kucheza? tunangoja kuona.
"Lakini naweza kusema kwamba anaendelea vizuri, anafuatilia matibabu kwa makini. Ana daktari wake binafsi. Nadhani hili linawezekana."
Fernando alikuwa akifanya mazungumzo na daktari wa Hispania sambamba na wafanyakazi wetu. "Tunajua jinsi hali ilivyo, na lazima tukabiliane nayo.
"Tunahitaji kufanya mambo mazuri kwa wachezaji wetu, na pia tunahitaji kufanya mambo mazuri kwa timu.
Torres ameshauriwa na mtaalam wa Hispania kupumzika kwa muda wa wiki tatu.Lakini kocha wake, anasisitiza kuwa pamoja na maagizo hayo haina maana kwamba aache kabisa kucheza.
No comments:
Post a Comment