Wednesday, November 4, 2009

Zain kuwaleta Yassou N'Dour na Angelique Kidjo

Na Jacqueline Massano

WANAMUZIKI Yassou N'Dour (Senegal) na Angelique Kidjo wa Benin wanatarajia kutoa burudani katika tamasha linalotarajia kufanyika Novemba 15 mwaka huu kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Zain, Costantine Magavilla alisema tamasha hilo limeandaliwa na mtandao huo kwa ajili ya kutoa burudani kwa watanzania.
Alisema lengo la kuandaa tamasha hilo ni kwa ajili ya kutoa burudani kwa watanzania ili nao waweze kupata nafasi ya kuburudika baada ya miangaiko ya hapa na pale.
Magavilla alisema wanamuziki hao ambao ni tishio Afrika wanatarajia kuwasili nchini wiki ijayo tayari kwa tamasha hilo.
Alisema kuwa tamasha hilo ambalo litakuwa ni maalum litakuwa la 'live' ili kuwapa raha wapenzi wa muziki.
"Hawa ni miongoni mwa wanamuziki maafuru sana duniani, na ninaimani ujio wao utakuwa ni furaha kubwa kwa watanzania ambao hawajawahi kuwasikia wala kuwaona," alisema

No comments:

Post a Comment