Thursday, November 5, 2009

Kocha Nigeria amuita Uche

ABUJA, Nigeria

KOCHA wa Nigeria Shaibu Amodu amelazimika kumuita kiungo Kalu Uche katika kikosi chake kwa ajili ya mchezo muhimu wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Kenya utakaofanyika Novemba 14.
Sani Keita alilazimika kujitoa katika kikosi hicho kwa sababu ya maumivu ya mgongo, ambaye awali aliachwa katika kikosi hicho, alichukua nafasi yake.
Uche amejiunga katika kikosi ambacho pia wamo nyota wa Chelsea John Obi Mikel.Kiungo huyo hivi karibuni alikosa mchezo dhidi ya Msumbiji na hajaichezea klabu yake katika mwezi wote wa Oktoba.

Kikosi kamili:
Makipa:
Dele Aiyenugba (FC Bnei Yehuda, Israel), Greg Etafia (Moroka Swallows, South Africa) na Vincent Enyeama (Hapoel Tel Aviv, Israel)Mabeki: Dele Adeleye (Sparta Rotterdam, Holland), Onyekachi Apam (Nice, France), Elderson Echieljile (Stade Rennes, France), Obinna Nwaneri (FC Sion, Switzerland), Chidi Odiah (CSKA Moscow, Russia), Daniel Shittu (Bolton Wanderers, England), Taye Taiwo (Olympique Marseille, France) na Joseph Yobo (Everton, England)Viungo: Olufemi Ajilore (FC Groningen, Holland), Yusuf Ayila (Dinamo Kiev, Ukraine), Kalu Uche (Almeria, Spain), John Obi Mikel (Chelsea, England) na Seyi Olofinjana (Hull City, England)
Washambuliaji: Yakubu Aiyegbeni (Everton, England), Joseph Akpala (FC Brugge, Belgium), Michael Eneramo (Esperance, Tunisia), Nwankwo Kanu (Portsmouth, England), Obafemi Martins (Wolfsburg, Germany) Obinna Nsofor (Malaga, Spain) na Osaze Odemwingie (Lokomotiv Moscow, Russia)

No comments:

Post a Comment