
LIVERPOOL iliyomatatani ilitoka sare ya 1-1 na Olympique Lyon jana, na kuiacha timu hiyo katika hatari kubwa ya kutolewa mapema katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, wakati Inter Milan ikiibuka na ushindi katika mchezo wake.
Mabingwa hao wa Italia walifunga mara mbili dakika tano za mwisho na kuifunga Dynamo Kiev 2-1 ugenini na kupata ushindi wake wa kwanza katika mechi za Ulaya.
Pointi moja ya Lyon ilitosha kabisa kuipeleka timu hiyo katika hatua ya 16 bora pamoja na Sevilla, ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na VfB Stuttgart, wakati timu hizo mbili zikiungana na Manchester United, Chelsea, Girondins Bordeaux na Porto kucheza hatua ya mtoano.
Mabingwa wa Ulaya Barcelona, wiki mbili zilizopita ilifungwa nyumbani 2-1 na Rubin Kazan, juzi ilibanwa na kulazimishwa suluhu ugenini na Warussia hao katika mchezo uliofanyika kwenye baridi kali, na sare hiyo kuwaweka babaya mabingwa hao watetezi.
Arsenal, ilipata mabao mawili kutoka kwa Cesc Fabregas, wakati ikiibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya AZ Alkmaar .
Mabingwa mara tano wa Ulaya Liverpool ilisafiri hadi Lyon iliyopoteza mechi sita kati ya saba zilizopita katika mashindano yote, ikiwemo kipigo cha 2-1 kwa Lyon katika mchezo uliofanyika Anfield, na katika mchezo huo wa juzi walimkosa nahodha wao majeruhi Steven Gerrard.
Liverpool walifikiri wangeweza kuibuka na ushindi wakati Ryan Babel alipofunga bao na kuiweka mbele timu hiyo kwa shuti la juu kutoka umbali wa mita 25 katika dakika ya 83.
Lakini, mshambuliaji wa zamani wa Racing Club na Porto Lopez aliwafungia wenyeji bao la kusawazisha katika dakika za mwisho.
No comments:
Post a Comment