VIPIMO jijini Amsterdam vimeonyesha kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anahitaji wiki mbili zaidi za matibabu ili kuponya jeraha lake katika kifundo cha mguu, ilisema klabu hiyo inayoshiriki La Liga.
Ronaldo, ambaye hajacheza tangu alipoumia wakati alipokuwa akiichezea Ureno ikiibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Hungary Oktoba 10, alitarajia kurejea uwanjani hivi karibuni.
Lakini Real ilisema vipimo alivyofanyiwa Jumatano na daktari huko Amsterdam, Uholanzi aliyemtibu kifundo hicho hicho cha mguu mwaka jana alithibitisha kuwa mchezaji huyo anahitaji wiki mbili zingine kwa ajili ya matibabu kabla hajarejea uwanjani.
Alirejea kuwasiliana na daktari, Niek van Dijk, huko Amsterdam katika siku 15, waliongeza katika taarifa yake ya mtandao (http://www.realmadrid.com/).
Ronaldo anajiandaa kukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya wapinzani wao wa jiji Atletico Madrid pamoja na ule wanaotaka kulipiza kisasi cha kufungwa 4-0 dhidi ya timu ya daraja la tatu ya Alcorcon Jumanne katika mchezo wa Kombe la Mfalme katika mchezo wa pili wa timu 32 bora kwenye uwanja wa Bernabeu.
Shirikisho la Soka la Ureno jana ilitupilia mbali taarifa ya huko Hispania katika gazeti la michezo la kila siku la Marca lilisema kuwa jeraha hilo linahitaji anagalau mwezi mwingine kwa ajili ya kupona, na kumlazimu Ronaldo kuwa nje katika mechi za marudiano za Kombe la Dunia dhidi ya Bosnia.
"Atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu endapo atafanyiwa upasuaji, lilisema gazeti hilo."Hata Marca lilipata taarifa potofu, "alisema kiongozi wa shirikisho la soka Gilberto Madail, akiongeza kuwa ana matumaini Ronaldo atacheza dhidi ya Bosnia huko Lisbon Novemba 14 na siku nne baadae huko Zenica.
"Ronaldo anataka kucheza, atajiunga na kikosi cha wachezaji wenzake na atafanyiwa uchunguzi na jopo la madaktari.


No comments:
Post a Comment