Na Badru Kimwaga
KLABU ya soka ya Simba imetangaza kuvunja kambi ya visiwani Zanzibar na kurejea jijini Dar es Salaam ambapo kesho inatarajia kuendelea na mazoezi yao kwenye dimba la Kinesi, ili kujiandaa na mechi yake na Mtibwa Sugar.
Uongozi wa Simba umesema umeamua kuvunja kambi hiyo ya Zenji kwa vile kazi iliyowapeleka huko imeisha kwa kuzichakaza timu za Azam na Yanga zilizokuwa zikiwapa presha kabla ya kukutana nazo katika ligi kuu nchini.
Mhazini Mkuu wa Simba, Almas Chano, amesema, kambi ya Simba imeamua Dar na kesho ndio wachezaji wataanza mazoezi baada ya kupewa mapumziko kwa kuiua Yanga baoa 1-0 katika mechi yao ya Jumamosi.
Chano alisema mazoezi yao yatakayofanyika kwenye uwanja wa Kinesi ni maalum kwa ajili ya pambano lao lijalo dhidi ya Mtibwa Sugar kabla ya ligi kwenda mapumziko hadi mwakani, ingawa wao wataendelea kujifua zaidi.
"Ile kambi yetu ya Zenji, imevunja kimoja na sasa timu imehamia Dar ambapo Jumatano (kesho) timu itaendelea na mazoezi kwa ajili ya kumalizia mechi yetu dhidi ya Mtibwa ambayo tunataka pia tushinde," alisema.
Alisema katika mazoezi hayo ya kesho wanatarajia kuvionyesha hadharani vifaa vyao viwili vipya wanavyotaka kuvisajili katika dirisha dogo, akiwemo mchezaji mmoja kutoka Yanga, ambaye hata hivyo alikataa kumtaja jina lake.
Hata hivyo pamoja na Chano kukataa kumtaja jina kifaa hicho kipya toka Yanga, zipo taarifa kwamba klabu yao ipo mbioni kumnyakua beki Nadfir Haroub Cannavaro aliyekuwa Vancouver Whitecaps ya Canada.
Simba na Mtibwa zinatarajiwa kumenyana Novemba 10 kwenye dimba la Uhuru. Simba iko kileleni ikiwa na pointi 30, huku Mtibwa ikifuata kwa kuwa na pointi 19.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment