Sunday, November 8, 2009

Man Utd, Chelsea uso kwa uso leo

LONDON, England
WAKONGWE wa soka wa Ligi Kuu ya England, Chelsea na Manchester Unitedb, leo watashuka katika uwanja wa Stamford Brigde kutafuta pointi tatu muhimu.
Chelsea itaingia uwanjani ikiwa inaongoza ligi kwa kuwa na pointi 27 nyuma ya mahasimu wao wenye pointi 25 baada yakucheza michezo 11.
Vijana wa Chelsea watashuka dimbani wakijiamini kutokana na matokeo mazuri iliyoyapata hivi karibuni kwa kuzichapa Bulton, Blackburn na Atletico Madrid, hivyo itataka kuendeleza ushindi huo na kujikita kileleni.

No comments:

Post a Comment