Monday, November 9, 2009

Kipigo chamdatisha Ferguson

London, England
ALEX Ferguson, kocha wa mabingwa soka England, anaweza kujikuta kwenye adhabu ya kufungiwa kukaa kwenye benchi kufuatia kutoa kauli ya kumlaumu refa aliyechezesha pambano la dhidi ya Chelsea jana, Martin Atkinson.
Tayari kocha huyo wa Manchester United amekiri kusema maneno mabaya pale alimpomtuhumu refa Alan Wiley kuwa hana uwezo.
Lakini kwa kauli yake ya jana, ni wazi anajiandaa kukumbwa na adhabu nyingine akilalamika bao la ushindi lililofungwa na nahodha John Terry na kuifanya Chelsea kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi kali ya kupendeza.
Fergie alisema: "Wakati mwingine unakosa imani na waamuzi."Hivi ndivyo wachezaji wanavyosema. Ilikuwa ni pigo baya kwetu."Fergie alichukizwa na hatua ya refa kutoa adhabu ndogo iliyozaa bao pekee la ushindi kwa Chelsea.
Anadai kuwa, Didier Drogba ndiye aliyecheza rafu dhidi ya Wes Brown wakati akijaribu kuondosha mpira.
Alisema: "Darren Fletcher alikuwa na mpira, Ashley Cole akaruka juu na kupata adhabu ndogo, kisha Drogba akamsukuma Brown chini karibu na lango. Nadhani refa hakupaswa kulikubali goli."

No comments:

Post a Comment