Wednesday, December 9, 2009

Messi aongoza wanaowania tuzo

LONDON, England

NYOTA wa Barcelona Lionel Messi ana nafasi ya kuongeza tuzo ya mcheaji bora wa mwaka wa dunia wa FIFA katika zawadi yake ya mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya ya Ballon d'Or.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye atakuwa mchezaji wa kwanza wa Argentina kushinda tuzo hiyo, yumo katika orodha hiyo pamoja na mchezaji mwenzake wa Barcelona Xavi na Andres Iniesta.
Anayeshikilia tuzo hiyo Cristiano Ronaldo na nyota mwenzake wa Real Madrid Kaka ndio wanaokamilisha orodha ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo.
Mshambuliaji wa England Kelly Smith yumo katika orodha ya wachezaji wanmaowania tuzo kama hiyo kwa upande wa wanawake.
Messi, Xavi na Iniesta wanatengeneza muhimili wa timu ya Barcelona, na kuiwezesha timu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Primera Liga na Kombe la Ligi msimu uliopita.
Messi alipiga mpira wa kchwa uliopmpita kipa wa Manchester United Edwin van der Sar na kuiwezesha Barca kuibuka na ushindi wa bao 2-0 katika fainali iliyofanyika Rome nchini Italia.
Wiki iliyopita, Muargentina huyo alimbwaga Ronaldo kwa kura nyingi katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa Ulaya baada ya kupata pointi 473 dhidi ya 233.
Sasa mchezaji huyo anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya FIFA baada ya kuibuka wa pili nyuma ya Kaka katika kinyang'anyiro cha mwaka 2007 na alikuwa nyuma ya Ronaldo mwaka 2008.
Nyota wa England Steven Gerrard, Wayne Rooney, Frank Lampard na John Terry wote wameshindwa kuwemo katika orodha hiyo baada ya kuwemo katika kinyang'anyiro cha awali cha wachezaji 23 mwezi Oktoba.
England wanajisikia faraja baada ya mchezaji wao mmoja kuwemo katika orodha ya wachezaji wakike wanaowania tuzo hiyo ya mchezaji bora, Smith akiwa miongoni mwa wachezaji watano wanaowania tuzo hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye anacheza soka Marekani, alikuwemo katika kikosi cha England kilichofikia fainali ya Euro 2009.
Wachezaji wengine wanaowania tuzo hiyo ni mshindi wa mwaka jana Marta na Mbrazil mwenzake Cristiane, pamoja na Wajerumani wawili Inka Grings na Birgit Prinz.
Kura hizo hupigwa na manahodha na makocha wakuu wa timu za taifa za wanaume na wanawake.

1 comment:

  1. Ok, Ok
    Nimeiona njia ya hapa nilipokuwa kwa G-Sengo. Nami nikaona nivumbue kibaraza kingine. HONGERA SAANA kwa habari mbalimbali na hasa za michezo. Yaonesha wewe ni mwanaspoti mzuri na ni faraja kuona kinadada wamejidhihirisha hata huku
    Basi nikukaribishe kwenye ulimwengu huu wa changamoto na naamini utakabiliana nazo na kuendelea kutupa habari mbalimbali kuhusu mambo mbalimbali na hasa michezo ya nyumbani
    Baraka kwako na kwa wenye mapenzi mema nawe.
    Blessings

    ReplyDelete